Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haaland: Nimerudi nyumbani

Halandoo Pic Data Erling Haaland

Mon, 13 Jun 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Erling Haaland amesisitiza kuwa 'anahisi yuko nyumbani' katika klabu ya Manchester City baada ya uhamisho wake wa majira ya kiangazi akitokea Borussia Dortmund.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway, 21, amesaini mkataba wa miaka mitano na mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England baada ya miaka miwili na nusu ya kustaajabisha nchini Ujerumani.

Haaland alifunga mabao 86 katika mechi 89 alizocheza na Dortmund, na kuwasaidia kushinda DFB-Pokal, Mei 2021.

Fowadi huyo mahiri, ambaye alizaliwa Leeds, atafuata nyayo za babake Alf-Inge kwa kuiwakilisha City. Beki huyo wa zamani aliichezea klabu hiyo mara 47 mwishoni mwa maisha yake ya soka na alikuwa sehemu ya kikosi kilichopanda Ligi Kuu mwaka wa 2001-02.

"Yeye [Alf-Inge] aliishi Uingereza, aliichezea klabu," alisema Haaland katika mahojiano yake ya kwanza kama mchezaji wa City. "Ni kweli, mambo mengi yamebadilika katika miaka 20 iliyopita lakini aliishi hapa.

Klabu kadhaa ziliripotiwa kutaka kumsajili Haaland kabla ya kujiunga na kikosi cha Pep Guardiola, vikiwemo Barcelona, ​​Real Madrid na wapinzani wa ndani Manchester United. Hata hivyo alichagua kuichezea City.

"Nilizaliwa Uingereza, nimekuwa shabiki wa City maisha yangu yote," aliongeza Haaland. Nafahamu mengi kuhusu klabu. Nadhani mwisho, mambo mawili, Ninahisi niko nyumbani kidogo hapa. Pia nafikiri ninaweza kujiendeleza na kupata matokeo bora katika mchezo wangu nikiwa City."

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz