Nyota wa klabu ya Manchester City Erling Haaland kuelekea mchezo wao dhidi ya Liverpool ametanabaisha kuwa moja ya watu anaotamani kukutana nao ni nahodha wa Liverpool Virgil Van Dijk.
Haaland amemuelezea Van Dijk kuwa ndiye mlinzi mgumu zaidi na anapenda kukutana na walinzi wagumu ili apime uwezo wake halisi.
"Ni mtu muhimu sana Liverpool, nimemuona kwa muda mrefu.Anapambana sana na ni mtu poa.Ni jini lakini napenda kucheza mbele ya wachezaji kama yeye kwa sababu hapo ndio unapojipima na naweza kusema utakuwa mchezo mzuri." Alisema Haaland.
Manchester City itashuka dimbani jumapili hii ugenini kuikabili Liverpool kwenye dimba la Anfield na vita kubwa inatazamiwa kuwa kati ya Van Dijk na Haaland.