Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

HAL TIME: Yanga 1 - Ruvu 1, Santos aoneshwa kadi nyekundu

Yanga , Ruvu 1 1 Yanga vs Ruvu Shooting

Tue, 2 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maafande wa Ruvu wamekwenda mapumziko huku wakiwa wamecheza pungufu kwa dakika takriban 20.

Nahodha wao Santos Mazengo ameoneshwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi Fiston Mayele dakika ya 25.

Goli la Ruvu katika mchezo wa leo limefungwa na Shaban Msala 9', huku lile la kusawazisha likifungwa na Kiungo nyota kwa sasa nchini Feisal Salum kwa shuti kali la nje ya 18.

Golikipa wa Ruvu amefanya kazi nzuri mpaka sasa kwa kuokoa michomo mingi ya hatari.

Kwa mara ya kwanza Yanga imeruhusu goli tangu kuanza kwa msimu huu wa Ligi 2021/2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live