Kiungo wa timu ya Singida Fountain Gate, Nicolaus Gyan amerejea katika klabu hiyo ambayo awali aliondoka baada ya kuifungulia kesi ya madai ya ada ya usajili na malimbikizo ya mishahara.
Gyan alifungua kesi hiyo katika Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) ambayo alishinda na klabu hiyo kuamriwa kumlipa mchezaji huo.
Hata hivyo hivi karibuni mchezaji huyo ameonekana akifanya mazoezi na timu hiyo jijini Mwanza ambapo Ofisa Habari wa Klabu hiyo ametoa maelezo ni kwa nini nyota huyo amerejea.
Massanza amekiri klabu hiyo kudaiwa na wachezaji, tayari wamekaa nao wote na kukibaliana jinsi ya kuwalipa ndioyo sababu Gyan amerejea kikosini.
“Klabu imekaa na mchenzaji na kuchanganua madai yake na kukubaliana tutamlipa na tayari ameanza kulipwa, hivyo niwaambie tu wale walikuwa na maswali mengi, Gyan amerudi katika timu na ataitumikia hadi mkataba wake utakapoisha,” amefafanua Massanza.
Ameelaza kuwa hali ya amani imerejea katika klabu yao na wote wanaodai wasiwe na shaka malipo yao yatafanyika.