Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gwiji wa Soka Ujerumani Afariki Dunia

Franz Beckenbauer Mkongwe wa soka wa Ujerumani Franz Beckenbauer

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkongwe wa soka wa Ujerumani Franz Beckenbauer (78) anayetambulika kama moja ya wachezaji bora kuwahi kutokea, amefariki dunia.

Mlinzi huyo mahiri aliichezea Bayern Munich mechi 582 na kufikia kiwango cha juu kama mchezaji na Meneja.

Beckenbauer almaarufu kama “Der Kaiser” aliwahi kushinda ubingwa wa Ulaya mwaka 1972 akiwa kama mchezaji, vilevile alishinda Ballon d’OR mara mbili.

Mwaka 1974 alishinda Kombe la Dunia akiwa nahodha wa West Germany na mwaka 1990 alinyanyua tena kombe hilo akiwa Meneja.

Familia yake imetangaza msiba huo uliotokea jana na kusema kuwa Beckenbauer alifariki kwa amani usingizini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live