Tue, 3 Oct 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mshambulizi wa zamani wa Manchester City na timu ya Taifa England, Francis Lee amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79.
Lee amewahi pia kuwa mwenyekiti wa miamba hiyo ya Jiji la Manchester miaka ya 1990. Aliichezea Manchester City mechi 330 kati ya 1967 na 1974 akiifungia magoli 148.
Kupitia taarifa yake iliyomtaja nyota huyo kama ‘gwiji’ Manchester City imesema “Kwa huzuni kubwa na nzito tunatangaza kufariki kwa mchezaji wa zamani wa Manchester City na mwenyekiti Francis Lee.”
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: