Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gwiji: Tatizo Misri ni kocha

Egypt National Team Gwiji: Tatizo Misri ni kocha

Tue, 30 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Misri imetolewa katika hatua ya 16-Bora ya fainali za Mataifa ya Afrika 2023 baada ya kupoteza kwa penalti 8-7 dhidi ya DR Congo.

Mafarao hao walifuzu hatua ya mtoano baada ya mfululizo wa matokeo ya sare za 2-2 dhidi ya Msumbiji, Ghana, na Cape Verde katika kundi B, kabla ya kumaliza kwa sare tena dhidi ya DR Congo.

Kiujumla, kikosi hicho cha kocha Rui Vitoria hakikuweza kushinda mechi hata moja katika Afcon ya Ivory Coast na kinarejea nyumbani Misri kikiwa na sare nne huku kikuruhusu mabao saba, na kuwa moja ya kampeni za hovyo zaidi za Afcon kwa Mafarao hao katika historia ya hivi karibuni.

Akizungumza baada ya kipigo dhidi ya DR Congo, mshindi wa mataji matatu ya AFCON akiwa na Misri, gwiji Wael Gomaa alisema: “Tangu kuanza kwa michuano hii, nilisema kuwa tuna timu nzuri sana.

“Wastani wa umri wa kikosi cha sasa ni wa kutufanya tuweze kutwaa ubingwa. Nafasi zote zina wachezaji wazuri.

“Tumeteseka kutokana na uongozi mbovu wa kocha Rui Vitoria, ambaye anawajibika kwa wachezaji. Amewafanya wacheze ovyo na hakuwasaidia wacheze kwa ubora wao.

“Kiujumla, hili ndilo soka la ovyo zaidi kwa timu ya Misri nililopata kulishuhudia katika maisha yangu.

“Unaweza vipi kufuzu kwa sare? Hatukuweza kushinda mechi hata moja. ‘Sub’ zake pia hazina maana yoyote, kila anayeingia, hapakuwa na ubunifu katika kukabiliana na mechi.

“Njia yetu kwenda fainali ndiyo iliyokuwa nyepesi zaidi. Kama tungeshinda, tungeenda kukutana na Guinea.

“Lakini tumeajiri kocha wa kumfundisha soka la Afrika ambaye halifahamu kabisa. Tumeleta kocha wa kumfundisha namna ya kukabiliana na soka la Afrika.”

“Hii ni aibu na jina letu la Misri halistahili jambo hili. Kila aliyehusika na aibu hii anapaswa kuwajibika.”

Chanzo: Mwanaspoti