Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gwambina yafanya Kweli Nyamagana ikiichapa Mashujaa 2-1

Gwambina FC.jpeg Wachezaji wa Gwambina FC

Mon, 21 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Timu ya Gwambina imepata ushindi wao wa pili msimu huu baada ya leo kuichapa Mashujaa FC ya Kigoma mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi ya Championship.

Mchezo huo wa raundi ya 10 umechezwa leo kuanzia saa 10 jioni katika Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza ambapo Gwambina imepata mabao yake kupitia kwa George Komba dakika ya 34 na Charles Amlima wa Mashujaa akijifunga dakika ya 90 huku bao la Mashujaa likifungwa na Jeremanus Josephat mnamo dakika ya 40.

Huo ni ushindi wa pili kwa Gwambina msimu huu katika michuano hiyo huku michezo yote waliyoahinda wakicheza Nyamagana ambapo waliichapa Copco Veteran 3-0 na Mashujaa 2-1.

Gwambina inatumia Uwanja wa Nyamagana kwa mechi zake za nyumbani baada ya Uwanja wao wa Gwambina Complex kufungiwa na bodi ya Ligi kutokana na eneo la kuchezea kutokidhi viwango.

Timu hiyo inapata ushindi huo baada ya wikendi iliyopita kuchapwa mabao 4-2 na Ndanda FC ya Mtwara katika Uwanja huo.

Baada ya ushindi huo Gwambina imefikisha pointi saba na kusogea hadi nafasi ya13 wakitoka mkiani na kuzishusha Copco, Ndanda na Green Warriors, ambapo imeshinda michezo miwili, sare moja na kupoteza saba.

Chanzo: Mwanaspoti