Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gwambina, TFF ngoma ngumu

Gwambina Bundi.jpeg Gwambina, TFF ngoma ngumu

Sat, 24 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Pilato yupo mlangoni mwa Gwambina anangoja kuondoka na roho ya mtu baada ya timu hiyo kugomea Uwanja wa Nyamagana, Mwanza ikidai inaonewa kupelekwa michezo ya nyumbani katika uwanja huo.

Wiki iliyopita Gwambina ilikumbana na rungu la faini ya Sh2 milioni pamoja na kupokwa alama 15 baada ya kutofika uwanjani katika mchezo dhidi ya African Sports na wiki hii haijatokea uwanjani kucheza na Mbuni.

Gwambina inaburuza mkia ikiwa na alama saba kabla ya hapo ilishakumbana na faini ya Sh1 milioni kwa kuchelewa kufika uwanjani licha ya kuwa nyumbani.

Hata hivyo, inaelezwa hadi sasa wachezaji wengi wameondoka kambini kutokana na sintofahamu hiyo pamoja na ukata unayoikumba Gwambina.

Katibu wa Gwambina, Daniel Kirai alisema wachezaji wapewa ruhusa ya kutafuta timu na hilo lilikuwepo tangu awali waliwapa uhuru wachezaji wao.

“Wapo wachezaji waliondoka sababu tuliwaambia kama mtu atapata timu ambayo ina maslahi mazuri basi aje achukue barua na tuliwaambia mapema ili mradi maslahi yawe makubwa kuliko hapa.

“Kuna wachezaji wanne ndio tuliwapa ruhusa baada ya mchezo wetu ule wa FA wakaondoka lakini wengine bado wapo na hakuna niliyempa barua ya kumruhusu,” alisema Kirai.

Kuhusu suala lao na TFF alisema kama wao wanamakosa watawasubiri wawasikilize wanasemaje, kwanza itawapasa wajue wanakuja kufanya nini pia hatma ya ile michezo miwili na kuanzia hapo watajua wanakwendaje.

Hata hivyo, mmoja wa wachezaji ambaye alithibitisha kuondoka kambini alisema ni kutokana na ukata unaoendelea kwa sasa ndani ya timu hiyo.

Chanzo: Mwanaspoti