Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gurdiola ndio kikwazo cha Italia kufuzu Kombe la Dunia - Capello

Capello Fabio Capello

Sun, 27 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa zamani wa Italia Fabio Capello ameitahadharisha timu ya taifa hiyo kuacha kufuata mfumo wa soka la Hispania badala yake kufuata mfumo wa Ujerumani kwani hiyo ndiyo sababu ya kushindwa kufuzu kwenye fainali za kombe la dunia zinazotarajiwa kufanyika nchini Qatar,2022

Italia ambao ni mabingwa waa Ulaya kwa mwaka 2020,walikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Macedonia ya Kaskazini siku ya Alhamisi na kushindwa mara ya pili kufuzu kwenye fainali za kombe la dunia baada ya zile za mwaka 2018 zilizofanyika nchini Urusi kushindwa kufuzu kwa kufungwa na Sweden kwenye mchezo wa mtoano wa kufuzu kwenye fainali hizo.

“kwa zaidi ya miaka 15 soka la Italia limekuwa likiiga mfumo wa Pep Gurdiola,hatuchezi tena soka la nguvu wala hakuna pasi ndefu za kushambulia na wala hakuna uhitaji wa kufanya mabadiliko na nafikiri kwa sasa ni bora tukaiga mfumo wa mwalimu Jurgen Klopp”amesema Capello

Capello ambaye aliwahi kuvinoa vilabu vya Juventus,Real Madrid sambamba na timu ya taifa ya England ametolea  mfano kwa vilabu vya Atalanta na Fiorentina chini ya Vincenzo Italiano ambao wanatumia staili zinazoendana na Jurgen Klopp na kufanya vlzuri kwenye nyanja ya mashindano mbalimbali wanayoshiriki huku wakiiga mbinu ya soka la Ujerumani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live