Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gunners ndo wababe RCL 2023-2024

Wcdywtd Gunners ndo wababe RCL 2023-2024

Thu, 18 Apr 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Gunners FC ya jijini Dodoma imeibuka mabingwa wa Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) baada ya kupatab ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Hausung ya mkoani Njombe.

Mchezo huo wa fainali, umepigwa leo Aprili 17 kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma wa kusaka mbabe wa ligi hiyo ulitumiwa vyema na wenyeji.

Licha ya matokeo hayo, Gunners na Hausung zote zilishakata tiketi ya kucheza First League msimu ujao baada ya kumaliza katika nafasi mbili za juu.

Gunners waliokiwa wenyeji wa michuano hiyo iliyoshirikisha timu nane (Nane Bora) wanakumbukwa kwa historia ya kuwang'oa KenGold ya Ligi ya Championship katika michuano ya Kombe la Shirikisho hatua ya 64 na kutinga 32 Bora kwa bao 1-0 mchezo ukipigwa Sokoine jijini Mbeya.

Hausung inakumbukwa kwa ushindani waliouonesha dhidi ya Yanga, licha ya kulala 5-1 katika michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho.

Timu za Arusha City na Moro Kids zilizomaliza nafasi ya tatu na nne zitacheza play off ya kupanda daraja dhidi ya African Lyon na Kurugenzi FC zinazowania kubaki Fisrs League.

Chanzo: Mwanaspoti