Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gumzo: Miche Minnies ni mtoto wa Ronaldinho?

Miche Minnies.jpeg Gumzo: Miche Minnies ni mtoto wa Ronaldinho?

Mon, 4 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kufuatia kusambaa kwa picha za mchezaji wa Mamelodi Sundown mwanadada Miche Minnies mwenye umri wa miaka 21 ambaye amezaliwa Novemba 14, 2001, vyanzo mbalimbali vinaeleza kuwa kafanana sana na mwanasoka nguli duniani Ronaldinho ni kweli kw sababu ya muonekano wao kiujumla.

Miche amezua gumzo mitandaoni kwa sababu licha ya kufanana kwa muonekano na Rondaldinho, wanafanana mpaka staili ya kufuga na kufunga nywele, wanafanana mpaka staili ya uchezaji uwanjani, watu wanajiuliza, sio mtoto wa Dinho kweli huyu binti?.

Minnies amejitengeneza umaarufu katika soka la Afrika Kusini hasa kwenye Sasol League, kutokana na uwezo wake mkubwa wa kufumania nyavu uliomfanya amalize akiwa mfungaji Bora wa Ligi hiyo na kuisaidia timu yake ya wakati huo, Vasco Da Gama kutwaa ubingwa 2021.

Baadhi ya vyanzo zinaeleza kuwa Miche alizaliwa Heinz Park huko Afrika ya Kusini na ni raia wa taifa hilo lakini taarifa za wapi, eneo gani amezaliwa havijawekwa wazi kwenye tovuti rasmi ya klabu .

Miche kabla ya kujiunga na Mamelodi alikua nchini Brazil katika klabu ya Vasco da Gama na alimaliza kinara wa mabao huko kwa kuwa anahudumu nafasi ya mshambuliaji. Mwezi Agosti 2022 ndipo aliposajiliwa na Sundown Women's akitokea huko Brazil.

Kipaji chake kilimfanya akutane uso kwa uso na timu ya Taifa ya Wanawake ya Brazil mwaka 2018 kwenye mechi ya kombe la Dunia la Wanawake U17, lakini bahari mbaya alipata kisanga na kuondolewa kwa kadi nyekundu mapema tu kipindi cha pili na timu yake kupoteza kwa bao 4-1.

Vyanzo vingi vinaeleza kwa ufupi sana kuhusu familia yake na vingine havijaeleza kabisa, nimekuwekea picha ya baba yake kwenye comment ambayo kwa mujibu wa vyanzo ndio vinamtambua kama baba yake.

Watu wengi wanaotoa maoni yao kwenye mitandao ya kijamii hasa Twitter wanataka DNA test, wengine wakisema wanamtaka Gaucho atoke hadharani na kuielezea umma kwamba kwanini kafanana na huyu mchezaji.

Ni muhimu kujua kwamba Gaucho ana mtoto mmoja tu anayefahamika rasmi ambaye ni wa kiume aitwaye Joo Mendes. Alizaa na aliyekuwa mpenzi wake Janana Mendes, mwaka 2004.

Tangu ajiunge na Sundowns, Machi 2022 amefunga mabao 23 katika mashindano yote na kuisaidia timu yake kutetea ubingwa wa Hollywoodbets Super League. Pia walifanikiwa kufuzu michuano ya fainali za COSAFA Cup na CAF Women’s Champions League.

Kitu cha kustaajabisha ni kuwa hata profile ya mchezaji haipo official ya kumtambua huyu ni nani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live