Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guinea-Bissau yamtimua Kocha

Bacori Cande (8).jpeg Guinea-Bissau yamtimua Kocha

Sat, 10 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Guinea-Bissau haitaongeza mkataba wa kocha wake Baciro Cande baada ya fadhaa za fainali za Mataifa ya Afrika zinazoelekea ukingoni huko Ivory Coast.  Cande anaondoka baada ya miaka saba ya kuifundisha timu hiyo ya taifa.

Timu hiyo ilitolewa katika hatua ya makundi baada ya kupoteza mechi zote tatu, ikiwa moja ya timu mbili pekee kati ya 24 zilizoshiriki Afcon 2023 (pamoja na Gambia) ambazo hazikuambulia pointi hata moja. 

Kutemwa kwake kunahitimisha utawala wa Cande, ambaye mkataba wake unamalizika mwezi ujao. Baada ya kuteuliwa 2016, Cande aliiongoza Guinea-Bissau kufuzu fainali nne mfululizo za Afcon - ambayo ni rekodi kwa taifa hilo la Afrika Magharibi.

Lakini kocha huyo mwenye umri wa miaka 56 ameshindwa kushinda mechi hata moja kati ya 12 za fainali hizo chini ya utawala wake. Utawala wake umemalizika kinyonge zaidi Ivory Coast.

Cande ameungana na makocha kadhaa waliotupiwa virago baada ya fainali za Afcon 2023. Miamba kama Misri ilimtema kocha Rui Vitoria, pia Chris Hughton wa Ghana alitupiwa virago kama Djamel Belmadi wa Algeria pia alipoteza ajira.  Guinea-Bissau sasa inasaka mwanzo mpya baada ya kujengewa msingi imara na Cande.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live