Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guendouzi kurudi England

Mateo G Matteo Guendouzi

Fri, 14 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Aston Villa imeshaanzisha mazungumzo na Marseille kwa ajili ya kuipata huduma ya kiungo wa timu hiyo, Matteo Guendouzi, 25, katika dirisha hili.

Matteo ambaye aliwahi kuichezea Arsenal kabla ya kurudi Ufaransa baada ya kuonyesha vitendo vya utovu wa nidhamu, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028. Ni fundi wa boli ila nidhamu ni tatizo.

FULHAM inaangalia uwezekano wa kumsajili beki wa zamani wa Manchester United ambaye kwa sasa anaichezea Luton Town, Teden Mengi, 22, katika dirisha hili.

Mabosi wa Fulham wanapambana kuziba pengo la Tosin Adarabioyo ambaye ameondoka katika dirisha hili kama mchezaji huru kujiunga na Chelsea, ambayo inaendelea kusajili nyota wengi.

BEKI wa Tottenham, Djed Spence, 23, anadaiwa kuwa kwenye hatua nzuri ya kujiunga na Genoa katika dirisha hili kwa mkataba wa mkopo ambao utakuwa na kipengele cha kumnunua jumla ikiwa timu hiyo itahitaji kufanya hivyo.

Spence ambaye msimu uliopita alicheza mechi 23 za michuano yote. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.

LICHA ya tetesi kudai kwamba anaweza kutimkia zake nchini England ambako Arsenal na Tottenham zimeonyesha nia ya kumsajili, mshambuliaji wa Athletic Bilbao, Nico Williams amesisitiza kwamba ana furaha kuendelea kusalia Bilbao na wala hafikirii kuondoka.

Katika msimu uliomalizika Nico alitoa asisti 17 na kufunga mabao manane katika mechi 37 za michuano yote.

ATALANTA imejitosa katika vita dhidi ya timu nyingine barani Ulaya ili kuipata saini ya kiungo wa Galatasaray, Nicolo Zaniolo, ambaye msimu uliomalizika alicheza kwa mkopo Aston Villa.

Hata hivyo, Villarreal ndio timu ya kwanza kuwasiliana na wawakilishi wa staa huyu na tayari imeshafanya vikao vya kujadili uwezekano wa kumpata. Nicolo hahitaji kurudi Galatasaray.

KOCHA mpya wa Bayern Munich, Vincent Kompany amedhamiria kusuka eneo lake la ulinzi, ambapo amependekeza pia jina la beki wa kati wa VfB Stuttgart na Japan, Hiroki Ito naye asajiliwe katika dirisha hili.

Mbali ya Hiroki, Kompany pia anahitaji huduma ya Joe Gomez kutoka Liverpool sambamba na Jonathan Tah wa RB Leipzig.

CHELSEA na Bayern Munich ni kati ya timu zinazotajwa kuwa bado zinahitaji huduma ya kipa wa Valencia na Georgia, Giorgi Mamardashvili, 23, katika dirisha hili.

Newcastle ambayo ilihitaji kumsajili tangu dirisha lililopita, imeachana naye baada ya kuambiwa anauzwa kwa Euro 35 milioni. Mkataba wa Giorgi unamalizika 2027.

Chanzo: Mwanaspoti