Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guede amchimba mkwara mzito Inonga

Joseph Guede Yanga Guede amchimba mkwara mzito Inonga

Wed, 31 Jan 2024 Chanzo: Dar24

Mshambuliaji mpya wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara ‘Young Africans’ Joseph Guede ametamba kwa kuwaonya mabeki wa timu pinzani akiwemo Inonga Baka anayekipiga Simba SC kwa kusema kuwa amekuja kufanya kazi na wala hatakuwa na huruma nao.

Utambulisho wa nyota huyo ulikuwa gumzo tangu juzi Jumatatu (Januari 29) baada ya Young Africans kuweka wazi kuwa kutakuwa na sapraiz kwenye mchezo wao dhidi ya Hausing FC wengi wakitabiri kuwa ni wakati umefika wa kumuona Mshambuliaji wao mpya kwa mara ya kwanza Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar.

Young Africans katika dirisha dogo imesajili wachezaji watatu ambao ni Shekhan lbrahim na Augustine Okrah hawa wote walicheza mechi za Mapinduzi Cup huku Guede akionekana kwa mara ya kwanza jana Jumanne (Januari 30).

Mshambuliaji huyo amesema kuwa, hajaja Tanzania kumuangalia mtu usoni kwani amekuja kufanya kazi yake huku ikiwa ni meseji kwa mabeki wa timu pinzani wakiongozwa na Inonga ambaye anakumbukwa kwa bato lake na mshambuliaji wa zamani wa Young Africans, Fiston Mayele.

“Kwangu niweke wazi simuhofii beki yoyote na wala sitaki kusikia ukimtaja beki yoyote kuwa labda namuhofia na wala nimemfuatilia mimi nachofahamu ni kutakiwa kutimiza wajibu wangu nikiwa kama mshambuliaji wa Young Africans.

“Nikiwa kama mshambuliaji nafahamu ni wazi kuwa natakiwa kuhakikisha kuwa nafunga mabao ya kutosha, nikisema nianze kumhofia beki wa wapinzani sasa itakuwa ni ngumu kwangu kufunga, nikiwa kama straika wao mabeki ndio wanatakiwa kuniogopa mimi,” amesema mshambuliaji huyo.

Guede anakuwa mchezaji wa mwisho kutambulishwa na Young Africans baada ya Shekhani lbrahim kuanza na aliyefuatia kuwa ni Augustine Okrah ambao wote kwa pamoja wameshaivaa jezi ya klabu hiyo na kuonekana tofauti na Guede.

Chanzo: Dar24