Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guede, Okrah wamkosha Gamondi

Okrah Guedeee Guede, Okrah wamkosha Gamondi

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Viwango vinavyooneshwa na nyota wa Yanga SC, Joseph Guede na Augustine Okrah, vimeonekana kumkosha zaidi Kocha Mkuu, Miguel Gamondi kiasi cha kusifia usajili wao.

Nyota hao jana walikuwa chachu ya ushindi wa magoli 5-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) hatua ya 32 bora uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, Guede alifunga magoli mawili kwa kichwa ambayo yote alimalizia pasi za Okrah.

Akizungumzia viwango vya Guede na Okrah ambao wamejiunga na kikosi katika usajili wa dirisha dogo msimu huu, Gamondi amesema: “Ni maendeleo, inategemea kwa kila mchezaji uwezo wake wa kuendana na wenzake, kwa straika na winga wanahitaji kuwafahamu wenzao.

“Leo nilitaka kuwaweka Aziz Ki, Joseph (Guede) na Okrah (Augustine) pamoja, kwa sababu wana vipaji vikubwa, lakini hawajacheza pamoja.”

Kuhusu Guede kuanza kufunga, Gamondi anasema: “Sikumpa presha, niliongea na Guede, nikamwambia unapaswa kufunga, nakusapoti, unajua wakati mwingine anakosa nafasi, mechi iliyopita aligongesha mwamba wa juu, nikamwambia tulia, magoli yatakuja.

“Kiukweli Guede ni straika mzuri, anafiti kabisa katika mfumo wetu wa uchezaji. Ni mzuri katika mipira ya juu, kimbinu ni mzuri pia, kwetu yeye (Guede) na Okrah usajili wao katika dirisha dogo ni mzuri sana.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: