Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guede, Mkude, Diarra watifuana Yanga

Yanga 1080x650 Guede, Mkude, Diarra watifuana Yanga

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Joseph Guede, Jonas Mkude na Djigui Diarra, wameteuliwa kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Aprili 2024 (NIC Player of The Month).

Tuzo hiyo inatolewa na Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwa kushirikiana na Klabu yetu ya Young Africans ambapo ilianza kutolewa Oktoba 2023.

Mkude amekuwa katika ubora wake hivi karibuni baada ya kupewa nafasi kucheza katika mechi za ushindani alikuwa kwenye kikosi cha Yanga kilichokomba pointi tatu dhidi ya watani zao wa jadi Simba.

Katika mchezo huo uliochezwa Aprili 20 2024 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 2-1 Simba. Mabao yalifungwa na Aziz KI na Joseph Guede kwa upande wa Yanga.

Bao la Simba lilifungwa na Michael Fred likiwa ni bao pekee la kufutia machozi kwenye mchezo huo.

Mashabiki na Wanachama wa Yanga ndiyo wenye jukumu la kupiga kura kupitia Application ya Yanga SC, ili kumpata mshindi wa tuzo hiyo.

Tangu kuanza kutolewa kwa tuzo hizo, washindi waliopita ni; Stephane Aziz Ki (Oktoba), Pacome Zouzoua (Novemba), Djigui Diarra (Desemba), Clement Mzize (Januari), Mudathir Yahya (Februari) na Aziz Ki (Machi).

Kila mshindi wa tuzo hiyo, amekabidhiwa kitita cha shilingi milioni nne kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live