Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guardiola na bata la maisha nje ya soka

Pep Guardiola Utetezi Guardiola na bata la maisha nje ya soka

Fri, 2 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Moja kati ya makocha bora duniani kwa sasa ni Pep Guardiola ambaye mwaka jana aliumaliza kwa kuchukua mataji matatu kwa pamoja akianza na Ligi Kuu England, FA na Ligi ya Mabingwa akiwa na Manchester City.

Guardiola ambaye kwa sasa anapambana kuisaidia timu hiyo kutetea mataji yote hayo anajulikana kama mmoja kati ya makocha wenye maisha yakipekee nje ya uwanja kutokana na pesa alizonazo na mshahara wa Pauni 19 milioni kwa mwaka anaoupata.

Kocha huyu anakula bata la kutosha na kumiliki vitu mbalimbali vya thamani. Leo tumekusogezea maisha yake ya kifahari nje ya soka.

NDINGA

Silver Bentley, GTX700- Pauni 200,000

Range Rover, Pauni- £150,000

Mercedes GLE-Pauni 80,000

Mini Cooper-Pauni 30,000

MAPUMZIKO YAKE

Baada ya kushinda mataji matatu mwaka jana, alifunga safari kwenda Egypt akiwa na familia yake.

Walitumia siku mbili kula bata huko na kufanya utalii kwenye Pyramid.

Mwaka 2022, alisafiri hadi kwenye visiwa vya Barbados akiwa na mkewe Cristina baada ya kuchukua ubingwa wanne wa Ligi Kuu nchini England.

Alionekana akiinjoi maisha kwenye moja ya fukwe zinazopatikana kwenye visiwa hivyo.

Mwaka huu pia alioneakana na mkewe kwenye boti ya kifahari, kisha wakaonekana kwenye moja ya migahawa maarufu Italia kwenye Jiji la Venice wakinunua vitu vya bei mbaya.

Baada ya kujiunga na Man City mwaka 2016, kabla ya kuanza kazi aliichukua familia yake wakaenda kwenye visiwa vya Ibiza, Hispania kuponda raha.

MIJENGO

Mwaka 2017 alinunua moja ya nyumba za bei mbaya Jijini Manchester, akitumia Pauni 2.7 milioni. Nyumba hii inapatikana maeneo ya Salford ipo kwenye mtaa ambao wanakaa watu matajiri. Ndani yake kuna bwawa la kuogelea na gym na kiwanja kidogo cha kufanyia mazoezi.

Pep pia ana mjengo ulichokuwa umbali wa futi 8,000 huko Pedarlbes, Jijini Barcelona ambayo aliinunua kwa Pauni 8.55 milioni mwaka 2021.

Mjengo huo ambao unapatikana maeneo ya milimani unamuwezesha Pep kuona karibia mji mzima wa Barcelona kwa kuangalia akiwa kwake.

MZEE WA MITINDO

Amekuwa akitambulika kutokana na mitindo yake mbalimbali ya uvaaji.

Katika kudhihirisha anapenda kuvaa mavazi mbalimbali yenye thamani kubwa, Pep anamiliki koti moja aina ya ‘hoodigan’, ambalo lilitengenezwa na Herno na linadaiwa kuwa na thamani ya Pauni 1,200.

Amekuwa akiingia na staili mpya kile mechi mara kadhaa ameonekana kuvaa mavazi makubwa zaidi ‘mabwanga’ na mwaka tisheti aina ya ‘MDCR’ ambayo bei yake inafiki shilingi laki mbili za kibongo.

Mapema mwezi huu alithibitisha anayempa mapigo ya kuvaa ni mkewe Cristina ambaye wakati anakutana naye alikuwa akifanya kazi kama mbunifu wa mamodo kwenye duka la Serra Claret, linalomilikiwa na familia yake na Pep kuna wakati alishawahi kuonekana kwenye tamasha lilioandaliwa na duka hilo akiwa kama modo.

SAA

Richard Mille (RM) RM 27-01 Tourbillon Rafael Nadal-Pauni 590,000.

RM 022 Tourbillon Aerodyne-Pauni £455,000

RM 010 ‘Manchester City’-Pauni £75,000

RM 004 All Gray, Pauni 150,000.

RM 67-02 watch - Pauni 228,000

Patek Philippe Annual Calendar Chronograph 5905P-Pauni £55,000

Rolex Cellini-Pauni and a £12,500

Chanzo: Mwanaspoti