Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guardiola kuwakosa Walker, Stones vs Arsenal Jumapili

Walker X John Stones Guardiola kuwakosa Walker, Stones vs Arsenal Jumapili

Sat, 30 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amethibitisha kuwa walinzi wake wawili Kyle Walker na John Stones watakosa mechi ya Jumapili ya Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Arsenal kwenye Uwanja wa Etihad.

Walker aliumia wikiendi iliyopita akiwa na timu ya taifa ya Uingereza ilipocheza na Brazil na wakapoteza kwa bao 1-0.

Katika mchezo huo Walker alilazimishwa kutoka nje kwenye dakika ya 19 baada ya kupata jeraha kwenye misuli ya paja.

Stones naye alicheza dakika zote 90 dhidi ya Brazil, lakini alidumu kwa dakika 10 tu katika sare ya 2-2 dhidi ya Ubelgiji baada ya kupata tatizo la paja wiki hiyohiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live