PEP Gurdiola ameripotiwa kwamba ataachana na Manchester City wakati mkataba wake utakapofika tamati 2025.
Mhispaniola huyo, Guardiola ameiongoza Man City kubeba mataji matatu makubwa ndani ya msimu mmoja kwa mara ya kwanza ndani ya msimu uliomalizika hivi karibuni wa 2022-23.
Lakini, muda wa Guardiola huko Etihad tayari unaelekea ukiongoni, ambapo mkataba wake wa sasa utafika tamati katika kipindi cha majira ya kiangazi mwaka 2025.
Na ripoti zinadai kwamba Guardiola atafungasha virago vyake na kuondoka Man City muda huo utakapofika. Hadi kufikia 2025, Guardiola atakuwa ametumikia Man City kwa miaka tisa.
Hata hivyo, haifahamiki ni kitu gani Guardiola atafanya baada ya hapo, huku wengi wakidhani anaweza kuhamia kwenye timu za kimataifa. Wakati Guardiola alipotua Man City mwaka 2016, ilitarajiwa kwamba amedumu England kwa miaka mitatu kabla ya kutimkia zake Italia.
Kwa wakati huo, Guardiola alikuwa anafikiria kuweka rekodi ya kuwa kocha pekee aliyeshinda mataji makubwa ya ligi katika Ligi Kuu Nne Bora wa Ulaya, ikiwa sasa amefanya hivyo kwenye La Liga, Bundesliga na Ligi Kuu England.
Lakini, kwa sasa inaelezwa mpango huo umebadilika baada ya Guardiola kusaini mkataba mpya Etihad, ambapo sasa mkataba wake utampeleka hadi miaka tisa, mmoja tu pungufu ya kufikia miaka 10.
Guardiola amekuwa kocha wa pili kwenye soka la England kubeba mataji matatu ndani ya msimu mmoja baada ya Sir Alex Ferguson kufanya hivyo akiwa na Manchester United katika msimu wa 1998-99.