Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guardiola awavaa Wachambuzi, apewa majibu ya kukera

Guardiola: 'Arsenal Wamerudi Kuwa Wagombea Wakuu Wa Ligi Ya EPL' Guardiola awavaa Wachambuzi, apewa majibu ya kukera

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Man City Pep Guardiola amewavaa wachambuzi wa kituo cha matangazo ya Televisheni cha Sky Sports kinachorusha mechi za ligi kuu nchini Uingereza ambao pia ni wachezaji wa zamani wa Ligi hiyo Gary Neville, Micah Richard na Jemie Carragher.

"Gary, Micah na Carragher hawajawahi kushinda Premier League 4 mfululizo wala kati yao hakuna aliyewahi kushinda makombe matatu ndani ya msimu mmoja" alirusha jiwe Guardiola kwa wachambuzi hao ambao wamekuwa wakosoaji wakubwa wa makocha.

Carragher akijibu mawe hayo ya Pep kwa wachambuzi alisema “Ningeweza kushinda hayo yote kama Liverpool ingekuwa inamilikiwa na Nation State (familia ya kifalme ya Uarabuni inayomiliki City) au Liverpool ingehusishwa na tuhuma za upangaji wa matokeo na kuvunja miiko ya usajili”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live