Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guardiola awafungia vioo Barcelona

Pep Guardiola.jpeg Pep Guardiola

Mon, 10 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya uvumi wa miaka mingi juu ya kurejea Barcelona, Meneja wa Manchester City Pep Guardiola ameweka wazi kuwa hatarejea Barcelona na kubainisha kuwa amefunga mlango kabisa juu ya uwezekano wowote wa kurejea katika klabu yake hiyo ya zamani.

Alipoulizwa kama mlango umefungwa kabisa kwa ajili ya kurejea Barcelona, alisema, “Ndiyo, mlango umefungwa,” kama ilivyonukuliwa na Fabrizio Romano

Guardiola amekuwa na mafanikio makubwa akiwa kocha wa Manchester City ambapo chini ya uongozi wake, timu hiyo imeshinda mataji sita ya Ligi Kuu ya England, mataji mawili ya Kombe la FA huku ikitwaa ubingwa wa Ulaya mara moja.

Mashabiki wengi na wachambuzi wa soka kwa muda mrefu wamekuwa na matumaini kwamba huenda siku moja akarejea kwenye klabu ambauo alipata mafanikio makubwa kama mchezaji na kocha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live