Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guardiola awa mbogo kisa Haaland

Guardiola X Haaland.jpeg Guardiola awa mbogo kisa Haaland

Tue, 17 Jan 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amekiri Erling Haaland apewe ushirikiano kila mechi aendane na mfumo asisahaulike sana mchezoni.

Haaland alipata nafasi chache eneo la hatari kwenye mechi ya Manchester Derby uliyochezwa wikiendi iliyopita, Man City ikipokea kichapo cha mabai 2-1. Hadi mpira unamalizika Haaland amegusa mipira mara 19 tu.

Lakini Guardiola amesisitiza Haaland anatakiwa apewe ushirikiano aendane na mfumo wa timu alete madhara eneo la hatari.

Haaland hajafunga bao katika mechi tatu mfululizo rekodi ambayo ni mbovu tangu alipojunga na Man City akitokea Borussia Dortmund dirisha la usajili la kiangazi.

Nyota huyo wa Kimataifa kutoka Norway amefunga mabao 27 katika mechi 21 alizocheza lakini Guardiola hakupendezwa na namna alivyokua akipata wakati mgumu katika mechi za hivi karibuni walizocheza.

"Ngumu sana Haaland mipira ya mwisho iliyokuwa sahihi, atafutiwe nafasi zaidi, aligusa mipira mara chache sana dhidi ya Man United, alikuwa kama wamemsahau hivi, kuna maeneo wanapaswa kutambua, Haalans ni mfungaji mzuri lakini mambo kama haya yanatakiwa kuzingatiwa," alisema Guardiola.

Wakati huo kiungo wa zamani wa aliyewahi kukipig Man City, Didi Hamaan aliweka wazi timu inacheza vizuri bila ya uwepo wa Haaland hata kama akifunga mabao 40 msimu huu.Lakini Guariola alisema endapo watacheza bila ya Haaland kupewa ushirikiano mechi itakuwa ngumu kwa upande wake.

"Bila shaka tumecheza vizuri na vibaya, nadhani tunatakiwa kumairika zaidi kutokana na kiwango chetu, nadhani tupo vizuri, tutatafuta pia njia ya kupata matokeo mazuri," aliongeza Guardiola.

Man City ilishindwa kupata matokeo katika tatu za mwisho walizocheza dhidi ya Everto, Southampton kabla ya Manchester Derby.

Mana City itacheza mchezo wao mwingine wa ligi dhidi ya Tottenham kesho kutwa huku Guardiola akiwa na matumaini ya kupata ushindi baada ya kuboronga

Chanzo: Mwanaspoti