Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guardiola avunja rekodi ya magoli EPL.

Guardiola Bielsa 1024x576 Pep Guardiola akiwa na Biesla

Wed, 15 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Klabu ya Manchester City, Pep Guardiola amevunja rekodi katika Ligi ya Primier baada ya kuwa meneja wa kwanza kufikisha magoli 500 kwa haraka zaidi akiwa na klabu moja.

Guardiola aliiongoza Manchester City hapo jana katika mchezo wa Ligi kuu na kuibamiza Leeds kwa goli 7-0 katika uwanja wao wa nyumbani wa Etihad.

Magoli ya Man City yalifungwa na Kelvin De Bruyne (32′ na 62′) aliyefunga mara mbili, Phili Foden (08‘), Jack Greash(13′), Riyad Mahrez(49′), John Stones(74′) pamoja na Nathan Ake(78’).

Goli la ufunguzi la Foden lilikuwa ndio goli la 500 kwa meneja Pep Guardiola katika mechi 207 akiwa na Man city na kuwa meneja wa kwanza kufikisha magoli 500 haraka zaidi.

Aliyekuwa anashikilia rekodi hiyo ni meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp aliyefanikiwa kufikisha magoli 500 katika mechi 234 na sasa akisimama katika nafasi ya pili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live