Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guardiola atamba kutetea ubingwa wa Ulaya

Guardiola Uefa(14).jpeg Guardiola atamba kutetea ubingwa wa Ulaya

Wed, 20 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Barani Ulaya Manchester City Pep Guardiola amesema itakuwa rahisi zaidi wa kutetea ubingwa huo kuliko ilivyokuwa mwanzo wakati wakipambana kwa muda mrefu kuusaka ufalme wa barani humo.

City walinyanyua taji lao la kwanza la Ligi ya Mabingwa kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Inter Milan mjini Istanbul mwezi Juni 2023, na hivyo kumaliza miaka mingi ya kukaribia kulitwaa.

Alipoulizwa kuhusu nafasi ya City ya kutetea taji hilo baada ya mechi yao ya kwanza ya Kundi G nyumbani dhidi ya Red Star Belgrade jana Jumanne (Septemba 19), Guardiola aliwaambia waandishi: “Itakuwa rahisi zaidi. Kigumu zaidi ni kushindana.”

Hata hivyo, Guardiola alisema wachezaji wake hawapaswi kujisikia raha na kuongeza: “Kwa jana ilikuwa hatua ya kwanza. Tumejaribu kupata pointi tatu za kwanza na tumefanikiwa.

“Ni muhimu wachezaji wasijisikie wametulia. Kwa klabu yetu kushinda Ligi ya Mabingwa ni jambo la ajabu, lakini kwa mtazamo ni klabu ngapi zimeshinda?

“Hatujafanya chochote kikubwa katika michuano hii kwa miaka mingi, , lakini tunajivunia sana kwa mafanikio ya kuwa mabingwa angalau mara moja.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live