Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guardiola ataka ubingwa wa nne mfululizo

Pep Guardiola.jpeg Pep Guardiola

Tue, 9 Apr 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesisitiza kwamba timu yake inatakiwa kucheza vizuri mechi za mwisho wa msimu huu ili kuchukua taji la nne mfululizo kwenye Ligi Kuu England.

Man City ipo nafasi ya tatu na alama 70, inahitaji kutetea taji lao kwa mara ya nne mfululizo msimu huu na kocha wao anaamini inawezekana ikiwa watachanga vyema karata zao katika mechi zilizosalia.

"Ndio, tuna nafasi kubwa, kuna timu tatu zinazogombania taji, naweza kusema ni vita ya timu ambazo hazijapishana sana kwenye pointi."alisema Guardiola alipoulizwa juu ya mbio za ubingwa.

Mbali ya vita waliyonayo matajiri hawa wa Jiji la Manchester kwenye EPL, pia wana shughuli nyingine kwenye Ligi ya Mabingwa ambako wapo robo fainali na wanatarajia kucheza dhidi ya Real Madrid, kesho.

Hata hivyo, kocha huyu anaamini timu yake imekuwa na mapungufu kwa sababu ratiba yao ni ngumu sana na wanacheza mechi nyingi kwa muda mfupi.

"Hatupo imara kama ilivyokuwa hapo awali, kuna utofauti mkubwa jinsi tunavyohama kutoka eneo letu kwenda kwa adui na hata tunavyocheza, lakini haya yote ni matokeo ya kucheza mechi kila baada ya siku tatu, tunakuwa tunafikiria sana na kufanya kazi kwa nguvu ndio maana yote haya yanatokea"

Man City ilifanikisha kushinda mabao 4-2 mbele ya Crystal Palace wikiendi iliyopita na ilikuwa ni kazi ya ziada iliyofanywa na kiungo wao Kevin De Bruyne aliyefunga mabao mawili ya mwisho wakati ambao mechi ilionekana kuwa ngumu.

Mabao hayo yalimuwezesha kufikisha mabao 100 akiwa na Man City na Guardiola alisema kama sio staa huyo kuna uwezekano mkubwa wangepoteza mchezo huo.

"Leo Kevin ndio ameshinda mechi, isingekuwa yeye labda tusingeshindwa,"alisema Guardiola.

Chanzo: Mwanaspoti