Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guardiola aponda kiwango cha Man City licha ya ushindi mnono

City Win 4 Man City wakishangilia ushindi dhidi ya New Castle

Mon, 20 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ua ushindi mnono wa goli 4-0 dhidi ya Newcastle United, kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema timu hiyo ilikuwa na kiwango kibovu ambacho hajawai kukiiona msimu huu katika mchezo huo uliopigwa St James Park nyumbani kwa Newcastle Leo Jumapili Disemba 19.

Man City ambao ni vinara wa EPL walianza ungwe ya kwanza wakiwa chini ambapo walisababisha Newcastle United kupata nafasi nyingi ambazo bahati nzuri hazikutumiwa vizuri.

City walianza kutupia nyavuni kwa bao la kwanza kupitia kwa Ruben Dias, Joao Cancelo, Raheem Sterling na Riyard Mahrez ambao wote wameshindilia ushindi mzito wa Manchester City ambao wanaweza kutwaa ubingwa wa Ligi kwa mara ya pili.

“Kiwango cha kipindi cha kwanza kilikuwa kibaya zaidi, hatukucheza vizuri”, alisema Pep Guardiola.

“Hatukuwa kwenye ubora wetu, hatukuweza kutembea na mchezo, tulipoteza na kugusa mpira vibaya”.

Ushindi huo unaifanya Manchester City kuwa kileleni mwa msimamo wa EPL wakati ambao tunaenda kwenye sherehe ya christmas ni mara ya tatu kufanya hivyo.

Newcastle inabakia nafasi ya 19 alama tatu pungufu ya timu iliyonafasi ya pili 17 Watford hata hivyo magoli ya kufunga na kufungwa ndizo zinaleta utofauti na Norwich City.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live