Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guardiola aongoza kinyang'anyiro Kocha Bora wa mwaka EPL

Pep Guardiola Man City F365 1 Meneja wa Man City, Pep Guardiola

Fri, 19 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Pep Guardiola wa klabu ya Manchester City aongoza orodha ya makocha wanaowania tuzo ya kocha bora wa mwaka wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu akimbatana na makocha wengine.

Guardiola atakua akichuana na makocha Eddie Howe wa Newcastle, Marco Silva wa Fulham, Robertp de Zerbi wa Brighton, Mikel Arteta wa Arsenal, pampja na Unai Emery wa klabu ya Aston Villa ikiwa ni makocha ambao wamefanya vizuri zaidi ndani ya msimu wa mwaka 2022/23.

Orodha hiyo imetolewa mapema jana na Makocha hao wakipewa nafasi ya kuwania nafasi ya kua kocha bora wa msimu, Hii inatokana na kazi kubwa ambayo wamezifanya kwenye timu zao ndani ya msimu na kuwekwa kwenye daraja hilo ambalo limewatofautisha na makocha wengine.

Kocha Pep Guardiola anapewa nafasi ya kutwaa tuzo hiyo kwa mara nyingine na hiyo ni kutokana na ubora ambao amekua nao na kufanikiwa kuiongoza timu yake kufanya vizuri zaidi, Lakini pia Manchester City wana kila dalili ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza mara ya tatu mfululizo.

Makocha kama Eddie Howe, Unai Emery, Marco Silva, pamoja Mikel Arteta nao wamekua kwenye kinyang’anyiro hicho kutokana na mabadiliko ambayo wameyafanya kwenye timu zao kama Eddie Howe ameifanya Newcastle kua moja ya timu tishio ndani ya Uingereza, Vilevile kwa Mikel Arteta ambaye ameifanya Arseal kugombea ubingwa kitu ambacho watu wengi hawakukitarajia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live