Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guardiola amtaja Haaland kujiunga Real Madrid

Pep X Haaland Pep Guardiola na Erling Halaand

Thu, 6 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amekana taarifa za Erling Haaland kuhusu mkataba wake ambao una kifungu cha kuuzwa na timu yoyote siku za usoni, Real Madrid ikihusishwa kuwa itamsajili licha kusaini mkataba mrefu.

Kauli hiyo aliisema baada ya Guardiola kumshuhudia straika huyo akipachika mabao mawili kwenye mechi ya Ligi Mabingwa Ulaya usiku wa kuamkia jana Man City ilipokuwa ikimenyana na FC Copenhagen na kuibamiza mabao 5-0.

Haaland amekuwa moto wa kuotea mbali kwasasa kwani amefikisha jumla ya mabao 19 katika mechi zote alizocheza msimu huu zikijumuishwa na Ligi Kuu England, huku kocha wake akisisitiza taarifa hizo sio kweli vyombo vya habari vinazusha tu.

Akizungumza baada ya mechi Guardiola amesema siku hizi taarifa za tetesi hazizuiliki kwani vyombo vya habari vinapenda kuzusha mambo na wameendelea kukabiliana nazo.

"Hizi ni tetesi vyombo vya habari vinapenda sana kuzusha, kila siku zinatupa tabu kuzuia, muhimu Haaland amefiti kwenye mfumo, nadhani anafurahi kwasasa, tunatumia kila jitihada kuhakikisha anabaki kwasababu hata mashabiki wanamkubali, lakini lolote linaweza tokea siku za usoni, lakini kwasasa ana furaha." alisema Guardiola.

Mabao mengine ya Man City yaliwekwa kimiyani na Riyad Mahrez, Julian Alvarez kabla ya mchezaji wa Copenhagem kujifunga kwenye mchezo huo.

Wikiendi iliopita Haaland aling'ara kwenye mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Manchester United alipoifungia timu yake 'hat-trick' vijana wa Guardiola wakiibuka na ushindi wa mabao 6-3 dhidi ya mahasimu wao kwenye uwanja wa Etihad.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live