Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guardiola ampendekeza De Zerbi Barca

De Zerbii (19).jpeg Guardiola ampendekeza De Zerbi Barca

Mon, 4 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Pep Guardiola ameripotiwa kumpendekeza Roberto De Zerbi kwenye kibarua cha kuinoa Barcelona - licha ya mwaka jana kumtambulisha kocha huyo wa Brighton kama mrithi wake sahihi Manchester City.

Kocha Guardiola, anayeinoa Man City kwa sasa alianza maisha yake ya ukocha huko Nou Camp - ambapo alibeba mataji ya kutosha kwenye zama zake hizo. Alishinda Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili na La Liga mara tatu kabla ya kwenda kujiunga na Bayern Munich na baadaye akatua Etihad.

Guardiola amepata mafanikio makubwa Man City ambako kwa msimu huu anafukuzia taji lake la nne mfululizo la Ligi Kuu England. Wakati huo, kocha Jurgen Klopp, mpinzani wake mkubwa kweye mbio za ubingwa, akiwa anainoa Liverpool, ametangaza ataachana na timu hiyo ya Anfield mwisho wa msimu.

Majina kibao ya makocha yanahusishwa na kazi hiyo ya kwenda kurithi mikoba ya Klopp, akiwamo De Zerbi.

Hata hivyo, Mundo Deportivo linadai kwamba Guardiola tayari wameshawaambia Barcelona waende kumchukua Mtaliano huyo wakati Xavi Hernandez, atakapoondoka mwisho wa msimu.

Kiungo wa zamani wa Liverpool, Xabi Alonso naye yupo kwenye rada za Liverpool, tena akipewa nafasi kubwa ya kukabidhiwa mikoba ya Klopp kutokana na kufanya vizuri huko Bayer Leverkusen, huku De Zerbi akiwekwa kwenye chaguo la pili endapo kama miamba hiyo ya Anfield itakwama kwa Alonso.

Na wakati De Zerbi akisisitiza kwamba anachofikiria kwa sasa ni Brighton tu na hajali hiyo ishu ya kuhusishwa na timu nyingine, kocha Guardiola amepanga kuwaambia Barcelona wamchukue kocha huyo.

Kwa mujibu wa Telegraph ni kwamba huko nyuma Guardiola aliwaambia wachezaji wa Brighton kwamba De Zerbi ni kocha ajaye wa Man City wakati timu hizo zilipokutana Mei 2022.

Lakini, baada ya hapo, Guardiola alisaini mkataba mpya Man City ambao utafika tamati 2025.

Chanzo: Mwanaspoti