KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kuwa wachezaji wake hawajalingana katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Burnley katika mchezo wa Jumamosi wa Ligi Kuu ya England wakati mchezo huo ukikosa baadhi ya furaha zake.
Mlipuko wa janga la virusi vya corona ulilazimisha msimu kuchelewa kumalizika na kubanana na kampeni ya sasa na mambo kuwa tofauti na ilivyozoeleka.
Man City, ambayo ilirejea kutoka katika kipigo cha wiki iliyopita kutoka kwa Tottenham Hotspur na kupanda hadi nafasi ya nane baada ya kuifunga Burnley, Jumanne, itasafiri hadi Porto katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kabla haijaikabili Fulham katika Ligi Kuu Jumamosi.
"Tatizo wachezaji wamepoteza furaha ya kucheza soka, “alisema Guardiola alipozungumza na waandishi wa habari.
"Kabla ya kuwa vizuri kucheza mara moja au mbili kwa wiki pamoja na viwanjani kuwepo na watazamaji. Sasa ni siku tatu na baadae nyingine tena. Tutasafiri kwenda Porto nakushinda, baadae tutajiandaa kucheza dhidi ya Fulham."
Man City imefunga mabao 10 katika mechi zake nane za mwanzo za Ligi Kuu ya England kabla ya mchezo wa Jumamosi walioshinda, na Guardiola alisema washambuliaji wake lazima wafanye kweli kama wanataka kurejesha mchezo wao katika timu.
"Mabao yametusaidia sisi. Gabriel Jesus anatakiwa kufunga mabao. Raheem Sterling wakati akicheza anatakiwa kufunga. Wanatakiwa kufunga mabao mengi. Kwanini wako hapa. Inategemea wachezaji, kiwango chao uwanjani, “alisema Guardiola.