Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guardiola: Ubingwa? unaondoka hivyo

Man City Pic Kocha wa Man City, Pep Guardiola

Tue, 7 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amekiri wamepoteza nafasi nzuri ya kuikaribia Arsenal kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England baada ya kupokea kichapo cha kushtua cha bao 1-0 kutoka kwa Tottenham Hotspur juzi Jumapili.

Man City ilikuwa na matumaini ya kupata ushindi kwenye mchezo huo ili kuipa presha Arsenal ambayo ilipokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Everton Jumamosi iliyopita.

Sasa Guardiola amekiri mbio za ubingwa msimu huu huenda zikawa zimeyeyuka, baada ya kichapo hicho na kwamba Man City imebaki nafasi ya pili ikiwa na pointi 45 tofauti ya pointi tano dhidi ya Arsenal yenye pointi 50.

Uwanja wa Tottenham umekua mgumu kwa Man City kwa mara nyingine kwani hawajapata matokeo mazuri katika mechi tano za mwisho walizokutana, huku chama hilo la Guardiola likishindwa hata kupata bao kwenye mchezo huo.

Guardiola alipoulizwa kama wamepoteza nafasi katika kinyang’anyiro cha kuwania ubingwa msimu huu Mhispania huyo alijibu: “Ndio bila shaka kwasababu Arsenal ilifungwa na kupoteza pointi, timu ilianza vizuri ilitakiwa tupunguze uwiano wa pointi, lakini tulifanya makosa, hatuwezi badili kwasababu imeshatokea, makosa kama haya yanajirudia sana, nimeshangaa sana hatukupata bao hata moja dhidi ya Spurs, siwezi kuzungumza kuhusu hilo sio jambo rahisi, hatupo katika nafasi nzuri za mbio za ubingwa. “

Man City ilipewa nafasi ya ushindi kwenye mchezo wao dhidi ya Tottenham lakini matokeo yake ikaangukia pua uwanja wa Tottenham kwa kipigo hicho.

Mabingwa hao watetezi wa ligi wapo nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi tatu dhidi ya Manchester United ambayo ipo moto kutokana na kiwango chao bora wanachoendelea nacho. Endapo Man United itapata ushindi kesho Jumatano dhidi ya Leeds United, itakuwa pointi sawa na Man City kwa tofauti uwiano wa mabao.

Man City ina kiporo kimoja dhidi ya Arsenal, ambapo mchezo huo utakachezwa Februari 15 mwaka huu utakuwa na upinzani mkali kwasababu kila timu haitakubali kupoteza pointi kutokana na ushindani uliopo kwenye msimmao wa ligi.

Chanzo: Mwanaspoti