Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guardiola: Rooney? Aje tu akitaka

Guardiola Rooney Guardiola: Rooney? Aje tu akitaka

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Pep Guardiola amemwambia gwiji wa Manchester United, Wayne Rooney kwamba anakaribishwa kwa moyo mmoja huko Etihad aende akaone vile Manchester City inavyofanya mambo yake.

Nahodha huyo wa zamani wa England, Rooney, 38, alisema angependa sana kwenda Etihad kuwa msaidizi wa kocha Guardiola. 

Na kocha huyo wa zamani wa Barcelona amesema siku zote milango ya Etihad itakuwa wazi kwa ajili ya Rooney, ambaye kwa sasa anajitafuta katika namna ya kuwa kocha bora.

Guardiola amependezwa kwa namna Rooney anavyomzungumzia licha ya mafanikio makubwa aliyopata akiwa mchezaji.

Alipoulizwa kuhusu Rooney, Guardiola, 53, amesema: "Sijui anaishi wapi. Cheshire? Hapo patakuwa karibu, anaweza kuja muda wowote, anakaribishwa sana."

Guardiola yupo England kwa miaka minane hivyo anafahamu umaarufu wa Rooney, ambaye pia alikuwa kocha Derby, Washington DC na Birmingham City.

Rooney alisema Guardiola ni kocha mzuri anayefaa kwenda kujifunza kwake. Straika huyo mstaafu alimtaja Mikel Arteta kwa kile anachokifanya kwa sasa kwenye kikosi cha Arsenal tangu alipochaguliwa 2019.

Arteta alitumikia miaka mitatu akiwa msaidizi wa Guardiola huko Man City. Rooney amesema: "Unaweza kuona kile Arteta anachokifanya, hapo unapata alijifunza vya kutosha kutoka kwa Guardiola na hilo halina mjadala."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live