Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guardiola: Nimefunga ukurasa wangu Man City

Pep Guardiola, Ms(1).jpeg Guardiola: Nimefunga ukurasa wangu Man City

Sun, 24 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola amesema “amefunga ukurasa” katika klabu hiyo ya Ligi ya Premia baada ya kushinda Kombe la Dunia la Vilabu.

City ilishinda Fluminense 4-0 siku ya Ijumaa na kunyanyua taji lao la tano la 2023.

Ilimaanisha Guardiola ameshinda kila taji lililopo tangu alipojiunga kama meneja mnamo 2016.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Guardiola, ambaye amebakiza miezi 18 katika mkataba wake, alisema kazi yake “imekwisha”.

Alisema: “Nimefurahishwa sana na ningependa kusema tulikuwa na hisia kwamba tutafunga ukurasa; tulishinda mataji yote, hakuna kitu kingine cha kushinda. Nilikuwa na hisia kwamba kazi imekamilika, imekwisha.

“Sasa ni wakati wa Krismasi, tunanunua kitabu kingine na kuanza kukiandika tena. Miaka minane iliyopita, imekwisha.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live