Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guardiola: 'Hatma ya kipa Ederson haijulikani'

Guardiola: 'Hatma Ya Kipa Ederson Haijulikani'.png Guardiola: 'Hatma ya kipa Ederson haijulikani'

Wed, 24 Jul 2024 Chanzo: Bbc

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anasema hana uhakika iwapo kipa Ederson atasalia katika klabu hiyo msimu huu.

Kipa huyo wa Brazil amekuwa akivutiwa na ligi ya Saudi Pro League.

Guardiola anasema mwishoni mwa msimu uliopita bado alimchukulia Ederson kama golikipa wake chaguo la kwanza, ingawa alimchagua Stefan Ortega katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid.

Akizungumza baada ya timu yake kushindwa 4-3 na Celtic katika mechi ya kirafiki huko North Carolina, Guardiola alisema: "Ningependa abaki lakini inategemea klabu nyingine.

“Sijui hali ilivyo. Hakuna watu waliowasiliana nasi kumhusu katika siku za mwisho. Ni suala la mazoezi, kuwa nasi hadi dirisha la uhamisho litakapokamilika tutaona.”

Ederson aliingia uwanjani wakati wa mapumziko wakati City ilipopoteza kwa Celtic huko Chapel Hill, mchezo uliokuwa wa ufunguzi wa mabingwa hao wa Premier League kabla ya msimu mpya.

Chanzo: Bbc