Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guardiola: Haaland atacheza hata asipokuwa fiti

Haaland Pep Guardiola Man City Guardiola: Haaland atacheza hata asipokuwa fiti

Fri, 31 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema yuko tayari kumchezesha mshambuliaji wake Erling Braut Haaland kwenye mechi dhidi ya Liverpool kesho Jumamosi hata kama hatakuwa fiti kikamilifu.

Haaland, 22, alikosa mechi za timu ya taifa ya Norwei kutokana na majeruhi ambayo aliyapata kwenye mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Burnley lakini vipimo vya Leo Ijumaa vinaweza kuwa na majibu kamili.

Hata hivyo, Man City itakosa huduma ya Phil Foden ambaye atakuwa nje kwa wiki tatu kutokana na majeruhi.

“Maisha ni uthubutu, muda mwingine ni lazima tuthubutu”, alisema Pep Guardiola kocha wa zamani wa Bayern Munich na FC Barcelona.

“Madaktari watasema, mchezaji mwenyewe atanambia kuwa anajisikiaje”.

Haaland tangia kujiunga Manchester City msimu uliopita amefunga magoli 42 kwenye mechi 37 ikijumuisha magoli 26 ya EPL.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: