Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guardiola: Biesla ni Kocha Bora kuliko mimi

Skysports Pep Guardiola Marcelo Bielsa 5336143 Guardiola: Biesla ni Kocha Bora kuliko mimi

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu wa kikosi cha Manchester City Pep Guardiola ameweka wazi kuwa kocha wa zamani wa Leeds ambaye kwa sasa anaifundisha timu ya Taifa ya Uruguay Marcelo Bielsa kuwa ni miongoni mwa makocha hatari zaidi Duniani.

Pep amesema kuwa kwa namna kocha huyo anavyopambana na anavyofundisha anaweza kubeba mataji mengi makubwa kama angekuwa anafundisha timu kubwa zenye kila kitu.

Guardiola ametolea mfano kama angepewa klabu kama Barcelona basi kocha huyo angebeba mataji mengi sana na yeye angeenda kuifundisha klabu ya Leeds asingeipandisha daraja kama alivyofanya Bielsa.

"Mpeni Barcelona na mtaona namna anavyoshinda mataji, nipeni mimi ile Leeds United, bado nitaendelea kusalia Championship, nisingepanda daraja." Pep Guardiola

Kwenye historia ya Pep Guardiola kuwa kocha mkubwa Duniani alipita kwenye mikono ya kocha Marcelo Bielsa na alimfuata nyumbani kwake kisha Bielsa akampa mbinu za namna ya kuwa kocha bora.

Hivyo hadi kesho Pep Guardiola ana husudu sana uwezo wa kocha Marcelo Bielsa na anaamini kuwa huyu ndiye kocha bora Duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live