Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guardiola: 'Arsenal wamerudi kuwa wagombea wakuu wa ligi ya EPL'

Guardiola: 'Arsenal Wamerudi Kuwa Wagombea Wakuu Wa Ligi Ya EPL' Guardiola: 'Arsenal wamerudi kuwa wagombea wakuu wa ligi ya EPL'

Sun, 8 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema Arsenal watakuwa washindani wa muda mrefu wa Ligi ya Premia, kabla ya timu hizo mbili kukutana katika ligi kuu siku ya Jumapili.

Arsenal, ambao walimaliza nafasi ya pili nyuma ya City mwaka jana, hawajafungwa kwenye ligi msimu huu.

Kikosi cha Guardiola kilishindwa na Wolves wikendi iliyopita lakini kiko pointi moja mbele ya The Gunners.

"Walikuwa wapinzani wakubwa msimu uliopita na watakaa hapo kwa muda mrefu," Guardiola alisema.Alipoulizwa kama Arsenal watakuwa wapinzani wa taji msimu huu, aliongeza: "Kweli, pamoja na Liverpool.

"Arsenal imerejea. Nilipokuwa mvulana mdogo na nikianza kama meneja Barcelona najua walipambana na timu ya Sir Alex Ferguson ya Manchester United."Halafu kwa miaka mingi hawakuwepo lakini sasa wamerudi.

"Unapoona kwenye kalenda inasema unaenda Emirates [unajua] ni ngumu zaidi."Arsenal wamepoteza mechi 12 zilizopita za ligi dhidi ya City na hawajapata ushindi wa ligi kuu tangu 2015.

Chanzo: Bbc