Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Griezman kumfuata Messi Marekani

Griezman Antoine Antoine Griezman

Fri, 8 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann, 32, yupo mbioni kuondoka kwenye timu yake hiyo ifikapo Januari mwakani na kutua kwenye Ligi Kuu ya Marekani ambako amepokea ofa kutoka timu mbalimbali ikiwemo na Inter Miami inayoitumikia Lionel Messi.

Atletico imeonyesha nia ya kumuachia straika huyo na tayari imedaiwa kuwa imeshapata mbadala wake ikiwa Griezmann ataamua kuondoka.

Mara kadhaa straika huyo amenukuliwa akisema kwamba ndoto yake siku moja ni kucheza Ligi Kuu ya Marekani pale atakapoondoka Ulaya.

Licha ya utayari wa kumuuza, Atletico imesisitiza kwamba inahitaji ofa nzuri itakayoweza kuwashawishi kufanya hivyo kwani bado ina mkataba na Griezmann hadi mwaka 2026. Atletico inamuangalia straika wa Juventus, Federico Chiesa, kama mbadala wa Griezmann.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live