Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Greenwood mbioni kutua Juventus

Manchester United Yawapa Pigo Kubwa Getafe Kwenye Sakata La Mason Greenwood Mason Greenwood

Sun, 5 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Juventus kwa sasa ndio inaongoza kwenye mchakato wa kuiwania saini ya mshambuliaji wa Manchester United, anayecheza kwa mkopo Getafe, Mason Greenwood, 22.

Timu nyingi zinatamani kuipata huduma ya Greenwood kutokana na kiwango alichoonyesha katika La Liga msimu huu akiwa na Getafe. Tangu atue, Greenwood amefunga mabao 10 katika mechi 31 za michuano yote pia ametoa asisti sita.

Timu mbalimbali ndani ya Hispania kama Barcelona na Atletico Madrid zimeonyesha nia ya kumsajili ingawa changamoto kubwa kwa sasa inaonekana kuwa ni bei yake.

Man United inahitaji zaidi ya Pauni 50 milioni kumuuza Greenwood ambaye ana mkataba wa kuwatumikia hadi mwaka 2025. Hadi sasa Man United haijafanya uamuzi juu ya hatma ya staa huyu ikiwa ataondoka ama atabaki baada ya kuondoka mwaka jana licha ya kutokutwa na hatia juu ya mashtaka ya unyanyasaji wa kijinsi yaliyokuwa yanamkabili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live