Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Greenwood ishu yake ni Mei

Mason Greenwood Brace Mason Greenwood

Sun, 3 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Hatima ya mshambuliaji Mason Greenwood kwenye kikosi cha Manchester United itafahamika mwishoni mwa Mei mwaka huu, imeelezwa.

Mmiliki mpya wa miamba hiyo ya Old Trafford, bilionea Sir Jim Ratcliffe amewataka wanaohusika na masuala ya kuhusu mshambuliaji huyo anayecheza kwa mkopo Getafe kwa sasa, kuhakikisha wanapata ufumbuzi wa jambo lake kati ya sasa hadi mwisho wa msimu.

Bosi huyo anataka kuzungumza na makundi ya mashabiki pamoja na maofisa wengine wakubwa kwenye klabu hiyo juu ya suala la Greenwood kabla ya kufikia uamuzi wa mwisho.

Kinachoelezwa, kocha Erik ten Hag amefungua milango ya kumkaribisha kikosi staa huyo, lakini kama tu jambo hilo litaungwa mkono katika kila idara.

Chanzo cha karibu kilifichua: "Jim Ratcliffe anataka jambo hilo limalizwe hadi kufikia mwishoni mwa Mei, ili ikifika kipindi cha usajili cha majira ya joto kila kitu kiwe kimefahamika.

"Kuna timu zinamtaka Mason ikiwamo Barcelona, lakini uhamisho huo hauwezi kuzunguzwa kwa sasa hadi hapo itakapofahamika hiyo mwisho wa Mei. Kwa sasa hivi, mambo yapo nusu nusu kuhusu Mason kurudi."

Tajiri Ratcliffe imeelezwa yupo tayari kuwarudisha kwenye kikosi Greenwood pamoja na Jadon Sancho. Mara ya mwisho Greenwood kuichezea Man United, ilikuwa Januari 2022.

Sancho naye kwa sasa yupo kwa mkopo Borussia Dortmund baada ya kutibuana na Kocha Ten Hag.

Tajiri Ratcliffe alisema: “Tutafanya uamuzi. Sifahamu kama Greenwood bado atahitaji kuwa nasi. Yeye ni mchezaji wa Man United na sisi tunawajibika na mambo ya soka. Tutafanya uamuzi.”

Chanzo: Mwanaspoti