Klabu ya Manchester United imemrejesha mshambuliaji wake wa kimataifa wa Uingereza Mason Greenwood kwenye kikosi ambacho kitatumika msimu ujao kwenye michuano mbalimbali.
Mason Greenwood ameonekana kwenye tovuti ya klabu ya Man United akiwa miongoni mwa wachezaji waliobakizwa kwajili ya msimu ujao, Huku wachezaji wengine wakiruhusiwa kuondoka ndani ya klabu hiyo jambo ambalo limeibua hisia kwa mashabiki wa klabu hiyo.
Kinda huyo ambaye amekua nje ya uwanja kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa kutokana na tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia ambao ulikua unamkabili, Lakini alifanikiwa kuachiwa huru kutokana na kukosekana kwa ushahidi kwa upande wa washitaki.
Kurejea kwa Mason Greenwood kwenye kikosi cha Manchester United ni furaha kubwa kwa mashabiki wa klabu hiyo, Kwani mchezaji huyo ana kipaji kikubwa na alikua anatazamiwa kufanya makubwa siku za usoni kabla ya kukutwa na tuhuma hizo.
Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag alishabainisha kua anamuhitaji Mason Greenwood kwakua ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa, Lakini akisisitiza maamuzi hayapo mikononi kwake hivo atahitaji kusubiri maamuzi kutoka ngazi ya juu kujua mchezaji huyo atabaki au ataondolewa.