Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Greenwood aitwa timu ya taifa Jamaica

Mason Greenwood Getafe.jpeg Mason Greenwood

Sat, 14 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Jamaica imemfungulia milango nyota wa Manchester United anayekipiga kwa mkopo Getafe, Mason Greenwood kama atakuwa tayari kubadilisha uraia kutoka England.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Jamaica, Heimir Hallgrimsson amethibitisha hilo.

Hallgrimsson alitamka maneno hayo kupitia mahojiano na waandishi wa habari akisisitiza kuwa ana mchakato mpya wa kujenga kikosi.

Greenwood ambaye kwa sasa anakipiga kwa mkopo Getafe ameshafunga bao la kwanza LaLiga tangu alipojiunga dirisha la usajili la kiangazi.

Mchezaji huyo anastahili kuchaguliwa na taifa hilo kwani ana asili ya Jamaica licha ya kuichezea timu ya wakubwa ya England, lakini anakidhi vigezo vya kubadili taifa kwa mujibu wa kocha huyo wa Jamaica.

Greenwood (22) anafikiriwa kuondolewa katika kikosi cha England na kocha Gareth Southgate kufuatia kesi iliyomkabili licha ya kufutwa na Mahakama ya Greater Manchester.

Nyota huyo hajajumuishwa katika kikosi ha England tangu aliporudishwa kikosini Septemba 2020 baada ya kukiuka kanuni za Uviko 19. “Sidhani kama mimi ni tofauti na makocha wengine duniani. Tungependa kuwa na wachezaji wenye vipaji katika timu yetu,” kocha huyo alijibu swali baada ya kuulizwa na wanahabari uwezekano wa Greenwood kubadili utaifa.

“Kama atakuwa fiti na kiwango chake kitaimarika itaisaidia Jamaica. Kila kocha anatamani kuwa na wachezaji wazuri. Bila shaka Greenwood anakaribishwa na mabegi yake, lakini sio jambo la busara kumzungumzia mchezaji ambaye hayupo hapa (Jamaica). Greenwood alihamia Hispania ili kuwa mbali na England baada ya kesi kwisha.

Chanzo: Mwanaspoti