Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Greenwood aachiwa kwa dhamana sakata la ubakaji

Greenwood Mason Greenwood

Wed, 19 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United, Mason Greenwood amechiwa huru kwa dhamana baada ya kuhudhuria mahakamamni kufuatia Sakata la keshi yake ya kubaka na unyanyasaji wa kijinsia.

Greenwood (21) anakabiliwa na mashtaka matatu ikiwemo kujaribu kubaka, udharirishaji na matumizi ya nguvu kwa mpenzi wake.

Winga huyo alipelekwa katika Mahakama Kuu ya Hakimu Mkazi jijini Manchester ambapo msemaji wa Mahakama alibainisha kuwa kibali cha dhamana tayari kimetoka kwa lakini kwa masharti.

Miongoni mwa masharti aliyopewa Greenwood ni pamoja na kutofanya mawasiliano ya aina yoyote ile na mashahidi wa tukio hilo ikiwemo mlalamikaji mwenyewe (Mpenzi wake).

Mchezaji huyo alikamatwa kwa mara ya kwanza mwezi Januari baada ya picha mnato na video kusambaa mitandaoni zikionesha namna anavyomnyanyasa kijinsia mpenzi wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live