Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Grealish akubali mambo magumu, Manchester City

Jack.jpeg Jack Grealish

Sat, 25 Dec 2021 Chanzo: eatv.tv

Kiungo wa kimataifa wa England Jack Grealish amesema maisha ndani ya klabu ya Man City yamekuwa magumu kuliko alivyotarajia, Kiungo huyo alijiunga na Manchester City mwanzoni mwa msimu huu akitokea Astoni Villa kwa ada ya uhamisho ya pauni million 100.

Jack Grealish mwenye umri wa miaka 26 ndio mchezaji wa England mwenye thamani kubwa zaidi, aliweka rekodi hiyo baada ya kununuliwa  na Manchester City akitokea Astoni Villa kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 100 ambayo ni zaidi ya bilioni 308 kwa pesa za kitanzania.

Grealish amezungumzia maisha yake ndani ya Manchester City tangu alipojiunga na mabingwa hao wa England na kuweka wazi kuwa mambo ni magumu tofauti na alivyotarajia,

"Nimefanya vizuri hadi sasa, nina mengi zaidi ya kufanya. Imekuwa ngumu zaidi kuliko vile nilivyofikiria itakuwa, bado ninajifunza na kuzoea nimesikia watu wengine wanachukua mwaka kuzoea hapa, labda itakuwa hivyo kwangu’’.

Kiungo huyo tayari ameshaitumikia Manchester City kwenye michezo 15 kwenye michuano yote na amefunga mabao 2 lakini pia kapiga pasi za usaidizi wa magoli (assist) 3.

Chanzo: eatv.tv