Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Granit Xhaka: Mnamsingizia, niliamua mwenyewe

Granit Xhaka.png Granit Xhaka: Mnamsingizia, niliamua mwenyewe

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo Granit Xhaka amefunguka kwamba ni yeye ndiye aliyeshinikiza kuachana na Arsenal kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi na sio mkewe kama ambavyo inaelezwa.

Xhaka mwenye umri wa miaka 31, alitumikia Arsenal kwenye mechi 297 na kupata umaarufu mkubwa kwenye kikosi hicho cha The Gunners.

Baada ya kudumu kwenye timu hiyo kwa miaka saba, hatimaye mkali huyo wa kimataifa wa Uswisi aliachana na Arsenal kwenye dirisha lililopita akienda kujiunga na Bayer Leverkusen.

Kulikuwa na ripoti kwamba mkewe Xhaka, mrembo Leonita Lekaj, ndiye aliyeshinikiza mumewe ahame, lakini mwenyewe amefunguka, akidai hakuna kitu kama hicho.

Xhaka na mrembo Leonita walikutana kabla ya staa huyo hajajiunga na Arsenal Mwaka 2016 walikutana wakati anakipiga Borussia Monchengladbach.

Baada ya kutua Leverkusen, Xhaka alisema: “Sijaja hapa Leverkusen kama bosi, bali nimekuja kupata changamoto mpya.

Niliona muda wangu wa kubaki Arsenal umekwisha baada ya miaka saba ya kuwa London. Nimekuja hapa nikiwa mwenye uzoefu kama mchezaji na mtu. Wachezaji wengine naweza kuwapa kitu cha kujifunza.”

Kwenye kikosi cha Leverkusen, Xhaka ilielezwa kwamba anakwenda kucheza kwenye kiungo wa chini, mambo yote yakianzia kwake tofauti na alivyokuwa akitumika huko Arsenal.

Wakati anaondoka, Kocha Mikel Arteta alisema kuhusu Xhaka: “Tunaagana na mchezaji mahiri na mtu tuliyekuwa tunampenda sote. Imekuwa safari bora kwa muda wote tulikuwa pamoja, amefanya kila kitu kwenye klabu hii.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live