Kocha wa zamani wa Chelsea Graham Potter yuko kwenye orodha ya makocha wanaopewa nafasi kubwa ya kuinoa klabu ya Napoli ya Italia.
Rais wa Napoli, Aurelio de Laurentiis anafatilia kwa umakini chaguo lake wakati huu wa mapumziko ya Ligi kupisha mechi za kimataifa.
Graham Potter na na kocha mwenzake wa zamani wa Chelsea Antonio Conte ndiyo makocha wanaopewa nafasi zaidi kuchukua nafasi ya Rudi Garcia ambaye ana mwendo mzuri wa matokeo toka kuanza kwa msimu huu.
Mfaransa huyo aliajiriwa baada ya kocha aliyeshinda taji la Ligi Kuu ya Italia msimu uliopita, Luciano Spalletti kuondoka baada ya kumalizika kwa msimu wa 2022/23.
Napoli kwa sasa inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Serie A, wapo nyuma kwa alama 7 dhidi ya vinara wa ligi hiyo AC Milan pia Napoli wako nafasi ya pili katika kundi lao la Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.