Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Goti lamtibulia beki

Goti Pic Data Goti lamtibulia beki

Tue, 30 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

BEKI Salum Chuku amejikuta akiwa katika wakati mgumu baada ya kuwa nje ya uwanja kwa takribani nusu msimu bada ya kuumia goti.

Chuku ambaye msimu uliopita alikuwa katika kikosi cha Nkana kinachoshiriki Ligi Kuu nchini Zambia aliwahi zichezea pia KMC  na Singida United, alipomaliza mkataba alishindwa kusaini mkataba mwingine baada ya kuwa majeruhi.

Akizungumza na Mwanaspoti, Chuku alisema sababu kubwa iliyomfanya ashindwe kuonekana katika Ligi yoyote ni kutokana na majeraha hayo.

"Niliumia goti nikiwa mazoezini hapa Tanzania, kwahiyo inakuwa ngumu kusaini katika timu ukiwa katika hali hiyo na ndio maana sionekani".

Chuku alisema "Hali yangu inazidi kuwa imara  nazani katika msimu ujao nitarejea nikiwa vizuri zaidi ya nilivyokuwa,".

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz