Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Goti lamliza beki Kagera, ahofia namba

Datius Peter QERF Datius Peter.

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa Kagera Sugar, Datius Peter amesema maumivu ya goti aliyopata na kumweka nje yamemvurugia mipango yake msimu huu kwani yamemtoa kwenye ubora na sasa anahofia namba kikosini.

Peter ambaye alicheza mechi 10 kati ya 12 za mwanzo chini ya Kocha Mecky Maxime aliumia goti Februari 16, katika mchezo dhidi ya Mashujaa alipogongana na straika Reliant Lusajo na kujikuta nje ya uwanja.

Nyota huyo ambaye alikuwa chaguo la kocha wa zamani wa Kagera Sugar, Mecky Maxime na wa sasa Fredi Felix ‘Minziro’ kwa sasa yupo nje akiuguza jeraha hilo huku nafasi yake ikizibwa na kinda Dickson Mhilu.

Datius aliliambia Mwanaspoti alikuwa katika kiwango bora na kuaminiwa na benchi la ufundi lakini kwa sasa anapaswa kuanza upya kujitafuta ili kurejesha namba yake.

Alisema matarajio yake ni baada ya mapumziko haya huenda akawa amepona kutokana na matibabu anayoendelea kupata chini ya daktari wa timu hiyo, Ally Malindi.

“Sikutegemea kuumia kufikia kiasi hiki, lakini nashukuru naendelea vizuri na hadi ligi irejee baada ya mwezi mmoja nitakuwa nimerejea uwanjani,” alisema Datius.

Beki huyo wa kupanda na kushuka alikiri itamchukua muda kuweza kurejea kwenye kiwango chake kutokana na jeraha alilopata na hata kupata namba haraka itamchukua muda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live