Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Goran akomalia mambo matatu Pamba FC

Goran Pamba Goran akomalia mambo matatu Pamba FC

Sun, 21 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa Pamba Jiji FC, Goran Kopunovic amekaa kambini kwa muda wa wiki moja mjini Morogoro na kuwasoma wachezaji kisha kusema ameona mwanga kwa vijana wake na anaendelea kukomalia mambo matatu kabla ya kuingia kwenye Ligi Kuu Agosti 16 wakiwa na moto mkali.

Goran aliyewahi kuzinoa Simba na Tabora United kwa vipindi tofauti, amesema ameona wachezaji wakiingia taratibu kwenye mfumo, huku akiwakomalia utimamu wa mwili, mbinu za kiufundi na mitindo wa kiuchezaji kwa nyota wa timu hiyo iliyorejea Ligi Kuu baada ya msoto wa zaidi ya miaka 20 tangu iliposhuka.

Akizungumza na Mwanaspoti, Goran alisema juu ya kambi iliyoanza Julai 15, anataka wachezaji wacheze soka la chini la pasi nyingi kama soka linalotumiwa na timu ya taifa ya Hispania ilivyooonyesha kwenye michuano ya Euro 2024.

Goran alisema siku zote yeye ni muumini wa soka la kisasa na anataka aonyeshe vipaji walivyonavyo wachezaji wake, huku akisisitiza kwamba kama wameweza Hispania wakiwa na vijana wadogo kwanini asifanye hivyo kwa kikosi alichonacho.

“Kitu cha kwanza tunachokifanyia kazi kwenye kambi yetu ni utimamu wa mwili (fitness) lazima wachezaji wawe fiti na timamu kwa kiwango cha juu. Pia technic na tactics, ndivyo vitu muhimu vitatu ninavyovifanyia kazi kwenye maandalizi yangu,” alisema Goran na kuongeza;

“Nimependa mazingira ya kambi nashukuru uongozi wachezaji wamefurahia hapa, hizi wiki mbili lazima tuzitumie vizuri kwa sababu tuna siku chache kabla ya kuanza ligi. Tangu wiki iliyopita naanza kuona taratibu wachezaji wanaanza kuelewa ninachotaka. Tuko kwenye mwelekeo sahihi, tunatakiwa kuwa na subira, kuamini na kufanya kazi kwa bidii. kila mchezaji anapaswa kujiamini na kuonyesha nia ya kufanya vizuri halafu benchi la ufundi litaamua nani aanze.”

Kocha huyo aliyerejea baada ya kufutwa kazi Tabora United msimu uliopita, aliwataka mashabiki kutokuwa na matumaini makubwa.

Chanzo: Mwanaspoti